Kwenye maisha yoyote ya mwanadamu anaeyaendea mafanikio au kuvuka hatua moja kwenda nyingine lazima amshukuru mwenyezi mungu kwa kila jambo. Hivyo basi sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa Mbingu na Ardhi 7 kwa kunijaalia kuvuka hatua hii muhimu katika maisha yangu pia namshukuru Mama Yangu Mzazi kwa kunilea kwenye Misingi Imara ya dini ya Kiislamu na kuweza kunipeleka shule kuanzia vidudu, msingi, sekondari mpaka namaliza elimu yangu ya chuo kikuu Mzumbe na ku hold bachelor of Laws (LL.B).
KIMSALES.BLOGSPOT.COM
Tuesday, 5 January 2016
Thursday, 2 July 2015
Saturday, 11 April 2015
Sunday, 29 March 2015
MVUA YAZIDI KUNYESHA MKOA WA MBEYA
Mvua yazidi kuwanufaisha wakulima jijini mbeya hali ambayo imepelekea sekta ya kilimo kukua na kuwanufaisha wakazi wa jijini mbeya na nje ya maeneo. Lakini hali hiyo ya mvua imeleta wakati mgumu hasa kwa wafanya biashara wadogo al- maarufu kama machinga kwa biashara zao kudorora japokuwa msimu wa sikukuu ya pasaka, na kupelekea kupoteza kipato kikubwa kwao.
Thursday, 1 January 2015
JK ATOA SALAMU ZA MWAKA MPYA
Mwaka wa
uchaguzi umeingia. Usiku wa kuamkia leo, Watanzania wameupokea mwaka
mpya 2015 huku tafakari kubwa ikiwa ni matukio makubwa yatakayotokea
mwaka huu, ukiwamo Uchaguzi Mkuu na kura ya maoni ya Katiba
Inayopendekezwa.Mbali na uchaguzi wa rais wa awamu ya tano,
wananchi wataamua ama kuipitisha au kuikataa Katiba Inayopendekezwa,
mambo ambayo wasomi, wanasiasa na wanaharakati wameonya kuwa yanatakiwa
kuendeshwa na kusimamiwa kwa weledi na umakini mkubwa.
Vilevile, kutokana na matukio hayo kugharimu fedha nyingi, wataalamu wa uchumi wanatabiri kuwa mwaka huu utakuwa mgumu na itakaowalazimu Watanzania kufunga mikanda zaidi.
Pia, macho na masikio ya wananchi yako kwa vyama vya upinzani ambavyo vimeungana na kuzaa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuona kama vitasimamisha mgombea mmoja wa urais na katika nafasi za ubunge na udiwani kama vilivyokubaliana, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Maandalizi ya uchaguzi huo yanaanza mwezi huu kwa wapigakura kuandikishwa upya katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, ambalo tangu mwaka 2009 halijawahi kuboreshwa na hivyo kusababisha wengi kushindwa kupiga kura katika uchaguzi wowote uliofanyika baada ya 2010.
Pengine jambo ambalo linasubiriwa kwa hamu na wananchi ukiacha Uchaguzi Mkuu na Katiba Mpya ambayo kampeni zake zitaanza Aprili 30, ni mchakato wa ndani ya vyama vya siasa wa kupata wagombea urais, hasa kutokana na mvutano ulioanza kujitokeza ndani ya CCM na mvutano unaotarajiwa ndani ya Ukawa.

Tuesday, 9 December 2014
ESCROW KUING'OA CCM UCHAGUZI MKUU 2015
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema licha ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuwadharau Watanzania na kuamini kwamba hawana madhara kwa ustawi wake, kashfa ya uchotaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow itaking’oa chama hicho madarakani.Kauli hiyo imetolewa wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kuchukua hatua kutokana na mapendekezo manane ya Bunge yaliyotolewa na Ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu ukaguzi maalumu wa malipo yaliyofanyika katika Akaunti ya Escrow, uliofanywa na Mdhibiri na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) iliyowasiliwa bungeni hivi karibuni.
Akizungumza alipowasili mjini Kigoma jana,
Kafulila alisema kuwa licha ya wananchi kukerwa na tabia ya wizi na
ufisadi wa mali ya umma, bado CCM imeendelea kuwadharau kwa vile
wananchi hao kila mara wanaunga mkono chama hicho.
“Watanzania wamechoka kulinda wezi na mafisadi,
ndiyo maana wakati wa mjadala wa IPTL bungeni nimepigiwa simu nyingi na
wananchi waliodai wapo nyuma yangu. Inatia faraja, nami nasema kashfa ya
escrow itaing’oa CCM madarakani,” alisema Kafulila.
Alisema nchi ipo njiapanda na hali ni mbaya kwa
vile licha ya uchumi kuporwa na watu wachache, Serikali imeshindwa
kuwachukulia hatua stahiki wahusika na kuwafikisha mahakamani.
“CCM imeshindwa kumng’oa fisadi mmoja na kumburuza
mahakamani. Sasa itawezaje kushughulikia matatizo ya Watanzania ili
kuwaondoa katika matatizo?” alihoji Kafulila bila kutaja jina.
Akizungumza na gazeti hili mbunge huyo aliwataka wananchi kuikataa CCM kama kweli wanapenda maendeleo ya dhati.
Alidai kwamba sakata la IPTL limemjenga kisiasa
kiasi kwamba anajisikia faraja kupigania masilahi ya umma na kuokoa
mabilioni ya pesa ili jamii inufaike na matunda ya nchi.
Wiki iliyopita, mjadala kuhusu uchotwaji wa fedha
katika Akaunti ya Tegeta Escrow uliligawa Bunge katika makundi mawili
lilipojadili Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),
kuhusu fedha hizo hoja ikiwa; ni nani mmiliki wa fedha zilizogawanywa
kwa watu mbalimbali?
Makundi yaliyodhihirika katika mjadala huo ni
kundi la upinzani na wajumbe wa PAC ambalo lilitaka viongozi wa Serikali
waliolegalega na kusababisha upotevu wa Sh306 bilioni zilizokuwa katika
Akaunti ya Escrow wawajibishwe.
Kundi jingine lilikuwa halioni kiongozi wa
kuwajibishwa kwa sababu fedha hizo hazikuwa za umma. Hili lilikuwa na
wabunge wengi wa CCM, wengi wakihoji mapendekezo yaliyotolewa na PAC
wakati hayamo katika mapendekezo ya CAG.
Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ramo Makani alisema
katika mahojiano ya PAC na CAG hakuna sehemu yoyote ambayo CAG
alithibitisha kuwa fedha zile zilikuwa za umma, bali limechomekwa
kinyemela na PAC. Jambo hilo lilimfanya Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe
kusimama na kutoa taarifa akisema kuwa katika mahojiano yao na CAG swali
la kwanza lilikuwa ni kutaka kujua kama fedha za escrow zilikuwa za
nani.
Wednesday, 27 August 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)