Leo tarehe 11 Aprili 2014 majira ya saa nne asubuhi jiji la Mbeya liligeuka kuwa uwanja wa maapambano kati ya jeshi la polisi na madereva wa boda boda jijini humo. Ghasia hizo zimetokana na mauaji yaliyotokea jijini hapo ya mmoja wa dereva wa boda boda ambaye kifo chake kimesababishwa na wivu wa kimapenzi.
Marehemu ambaye alikuwa miongoni mwa madereva wa boda boda katika kituo cha mafiati jijini hapo aliuwawa na watu wasiojulikana baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na kujeruhiwa sehemu mbali mbali za mwili wake.
Taarifa kutoka kwa Khalfan Lusinga, 21 anayefanya kazi ya kuosha magari eneo la mafiati jijini Mbeya anadai kuwa kifo cha marehemu kimetokana na wivu wa kimapenzi unaomuhusisha marehemu na mwanamke aliyekuwa mke wa marehemu kabla ya ndoa yao kutengana.
Mwanamke huyo amekamatwa leo baada ya kikundi cha madereva wa boda boda kuungana na kutaka kumuua mwanamke huyo kwa lengo la kulipiza kisasi cha kifo cha dereva mwenzao, polisi mkoani mbeya walifanikiwa kufika eneo la tukio maeneo ya Mwanjelwa kabla ya madereva hao kutimiza azma yao ya kutaka kumuua mwanamke huyo.
Polisi mkoani humo walifanikiwa kuokoa maisha ya mwanamke huyo ambaye alikuwa tayari mikononi mwa madereva wa boda boda hao. kutokana na hatua hiyo madereva wa boda boda walianzisha ghasia za kutaka kupambana na jeshi la polisi kwa lengo la kutaka warudishiwe mwanamke aliyeokolewa na jeshi la polisi. tukio hili limetokea leo jijini Mbeya na kusababisha jeshi la polisi kutumia mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia hizo zilizodumu kwa takribani masaa manne.
No comments:
Post a Comment