Wachezaji wa timu ya mchezo wa meza (pool table) chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Mbeya wakiwa wanajiandaa na mashindano ya mchezo wa meza kwa ngazi ya mkoa yanayotarajiwa kufanyika wikiendi hii ndani ya jiji la Mbeya katika viwanja vya Airport Pub.
Kwa mujibu wa kaptain aliyemaliza muda wake wa timu hiyo ya chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Mbeya anayefahamika kwa jina la Kelvin Mwita (a.k.a Kevoo) timu hiyo inajumuisha wachezaji nane (8) wakiwemo wachezaji wa kiume saba (7) na wa kike mmoja(1) anayejulikana kwa jina la Amina Muhina.
Maandaliizi ya timu yao yanaendelea vizuri na wapo tayari kushiriki na kuchukua ubingwa wa mashindano hayo yanayo dhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania TBL kupitia bia yao ya safari lager wakishirikiana na chama cha mchezo wa meza Tanzania (TANZANIA POOL ASSOCIATION).
Mashindano hayo yatafanyika jijini Mbeya mnamo tarehe 13 Aprili 2014 na yata jumuisha timu kutoka vyuo vikuu vitano vilivyopo ndani ya jiji la Mbeya.
Timu ya chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Mbeya kwa sasa watashiriki kwa mara ya nne katika mashindano haya, kwa mara ya kwanza mwaka 2011 waliibuka washindi wa pili kwa ngazi ya mkoa, kwa mara ya pili waliibuka washindi wa pili na kwa mara ya tatu mwaka 2013 waliibuka washindi wa kwanza kwa ngazi ya mkoa na washindi wa pili ngazi ya kitaifa.
Timu ya mchezo wa meza (pool table) ya chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Mbeya inaahidi ushindi katika ngazi zote kimkoa na kitaifa, mashindano ya kitaifa yatafanyika mapema mwaka huu ndani ya mkoa wa kilimanjaro wilaya ya Moshi mjini.
No comments:
Post a Comment