Tatizo kwa jamii: Angalia Shule iliyogeuka kuwa bwawa la samaki
Yala ni shule ya msingi iliyopo katika Kijiji
cha Yala Kata ya Luhanga Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na ipo umbali wa
kilomita 40 kutoka Barabara Kuu ya Mbeya-Iringa, ili kufika shuleni
hapo inakulazimu kutembea kwa mguu kutokana na magari na pikipiki
kushindwa kufika Shule hiyo ina muda wa zaidi ya miaka 20 tangu
kuanzishwa kwake, imezungukwa na mito minne ambayo imekuwa ikijaa maji
kipindi cha masika na kusababisha kukatika kwa mawasiliano na ukosefu wa
huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu. Kutokana na tatizo hilo la mito kujaa maji shule
hiyo imekuwa ikigeuka kuwa kisiwa na kusababisha wanafunzi na walimu
kushindwa kufika shuleni kwani mito hiyo haina madaraja ya kuwawezesha
kupita na kufika shuleni hapo.
Wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wamekuwa
wakitoka katika Vitongoji vya Mwashikamile, Ruaha, Waninyika, Mtakuja,
Yala na Lusaka na wote hushindwa kuvuka mito hiyo na kufika shuleni huku
walimu pia wakikumbwa na adha hiyo kutokana na shule hiyo kutokuwa na
nyumba za kuishi Walimu.Jairos Mpale ni Mwenyekiti wa serikali ndogo ya
maendeleo ya Mwashikamile katika Kijiji cha Yala anasema kuwa tatizo
hilo limekuwa kubwa zaidi kwa mwaka huu ukilinganisha na miaka
mingine
.Hii ni kutokana na mvua zinanyesha kwa wingi na wanafunzi
wamekaa nyumbani muda mrefu bila kwenda shule.“Watoto wetu wameshindwa kwenda shuleni hapo tangu
shule zote zilipofunguliwa Januari, kutokana na mito kujaa maji na kuna
mamba wengi na viboko hivyo ni vigumu kuvuka kwenda katika Shule ya
Yala na watoto wetu wamekosa masomo na hatujui ni lini wataanza masomo,”
anasema.
SOURCE: Mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment