Leo tarehe 17/5/2014 jiji la Mbeya lilipambwa na Tamasha kubwa kuwahi kutokea jijini humo linalohusisha vyuo vikuu zaidi ya vitano ikijumuisha uzinduzi wa vitabu, maonyesho ya kazi za sanaa za mikono, maonyesho ya mavazi, maonyesho ya ubunifu na usanifu majengo, pia uchezaji shoo na sarakasi vyote vikiambatana na michezo mbalimbali ya Mpira wa miguu, mpira wa wavu kwa upande wa timu ya wasichana kutoka chuo kikuu Mzumbe Mbeya waliibuka na ushindi dhidi timu ya chuo cha uhasibu Tanzania (T.I.A)
Saturday, 17 May 2014
TAMASHA LA VYUO VIKUU JIJINI MBEYA
Tamasha hilo lilienda sambamba na uzinduzi wa vitabu vya mwandishi Baraka A. Dishon ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Mbeya, pia kulikuwa na maonyesho ya usanifu wa majengo kutoka kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST), maonyesho ya sanaa za mikono, maonyesho kutoka Tamaduni music group, maonyesho kutoka Mtandao wa simu Smartcard, maonyesho ya mavazi, viatu na vyakula kutoka chuo kikuu Mzumbe Mbeya.
Tamasha hilo lilihusisha mchezo wa mpira wa miguu kati ya timu ya chuo kikuu Mzumbe na chuo cha uhasibu Tanzania( T.I.A) ambapo timu ya chuo kikuu Mzumbe Mbeya waliibuka na ushindi wa goli moja kwa upande wa wavulana, pia mashindano haya yalihusisha timu za wasichana kutoka chuo kikuu Mzumbe Mbeya kati ya kitivo cha sheria na Biashara ambapo kitivo cha sheria walibuka na ushindi wa magoli 3-1
Tuesday, 6 May 2014
RIPOTI YA CAG YACHACHAFYA CCM, CHADEMA
Bunge la Bajeti linaanza vikao
vyake kesho mjini Dodoma na moja ya kazi zake zitakazovuta hisia za
wengi ni Ripoti ya Mwaka 2012/13 ya Mashirika ya Umma na Taasisi za
Serikali itakayowasilishwa na Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG).
Pia, ripoti hiyo itakayowasilishwa keshokutwa
baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, kwa mara ya
kwanza itahusisha hesabu za vyama vya siasa nchini ambavyo kwa muda
mrefu vimekuwa vikidaiwa kutofanya ukaguzi wa hesabu zake.
Mawaziri waliotajwa katika ripoti hiyo ya 2012 ya
CAG na hivyo kushinikizwa kujiuzulu ni William Ngeleja (aliyekuwa
Nishati na Madini), Omar Nundu (Uchukuzi) na Naibu wake Athuman
Mfutakamba. Wengine ni Mustafa Mkulo (Fedha), Ezekiel Maige (Maliasili
na Utalii), Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii) na naibu wake, Dk
Lucy Nkya pamoja na Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara).
Vyama vya siasa
Ripoti hiyo pia itakuwa mwiba mchungu kwa vyama vya siasa ambavyo mwaka jana kwa nyakati tofauti Zitto alivinanga kuwa hesabu zake hazikaguliwi.
Zitto alifikia hatua ya kusimamisha ruzuku ya kila mwezi kwa vyama hivyo hadi vitakapowasilisha taarifa za ukaguzi wa fedha za umma tangu mwaka 2009 kwa Msajili wa Vyama vya Siasa. Katika maelezo yake, Zitto alisema tangu mwaka 2009 vyama tisa vya siasa vinavyopewa ruzuku na Serikali vilipata jumla ya Sh67.7 bilioni, lakini havijawahi kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa ruzuku kwa Msajili kama inavyopaswa kisheria.
Madai hayo ya Zitto yaliibua malumbano makali kati yake na viongozi wa vyama hivyo, kikiwamo Chadema, CUF na CCM ambavyo vilidai kuwa vimekaguliwa na wakaguzi binafsi na kuwasilisha hesabu hizo katika Ofisi ya CAG.
Sakata hilo liliingiliwa kati na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi aliposema kuwa hatazuia ruzuku ya vyama vya siasa kutokana na mkanganyiko wa ukaguzi uliojitokeza na kwamba kufanya hivyo itakuwa ni kukiuka sheria.
Uamuzi huo pia uliafikiwa na Kamati ya PAC ambayo awali, ilimwagiza Msajili huyo kusimamisha ruzuku hiyo hadi hapo vyama hivyo vitakapokuwa vimekaguliwa hesabu zao.
SOURCE:Mwananchi.co.tz

Saturday, 3 May 2014
WANAFUNZI WAWILI WA CHUO KIKUU MZUMBE MBEYA WAPOTEZA MAISHA
Wanafunzi wawili Albert Shenkelwa 23, na Michael Tarimo 22 wote wakiwa wanasoma kitivo cha biashara (DBA), wamepoteza maisha jana tarehe 02/5/2014 alasiri wakiwa wameenda picnic kwenye bwawa la Ifisi lililopo Mbalizi jijini Mbeya . Baada ya mmoja wao kutumia mtumbwi na kuzama kwenye tope ambapo mwenzake alijaribu kumuokoa bila mafanikio ndipo mauti yakawakuta wote wawili. Picha za wanafunzi wa Chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Mbeya wakiwa wanasubiri kuaga miili ya marehemu leo majira ya mchana katika viunga vya chuo.
Maiti zimesafirishwa kwajili ya mazishi ambapo Albert atazikwa Lushoto mkoani Tanga na Michael atazikwa jijini Dar Es Salaam. hili ni pigo kubwa kuwahi kutokea chuo cha Mzumbe kampasi ya Mbeya kwa kupoteza wanafunzi wawili kwa wakati mmoja. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIBARIKIWE. Kimsales blog team wanatoa salamu za pole kwa familia za marehemu na wote walioguswa na msiba huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)