KIUNGO, Yaya Toure, amechaguliwa kuwa Mwanasoka
Bora wa Mwaka wa Afrika ikiibuka kwa mara ya tatu mfululizo na kuwabwaga
mastaa kadhaa akiwamo Mnigeria, John Obi Mikel.
Kwenye tuzo zilizofanyika mjini Lagos, Nigeria
juzi Alhamisi usiku, kiungo huyo wa Manchester City alimpiku staa
mwenzake straika, Didier Drogba ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu ya chelsea ya na timu ya taifa ya Ivory Coast
Kwa kutwaa tuzo kwa miaka mitatu mfululizo, jambo
hilo limemfanya Toure, 30, kufikia rekodi za Abedi Pele na Samuel Eto’o
waliowahi kufanya hivyo huko nyuma.
Mikel ameshindwa kumshinda Yaya Toure na kuifariji
Nigeria ambayo mara ya mwisho kwa nyota wake kutwaa tuzo hiyo ilikuwa
mwaka 1999 wakati fowadi, Nwankwo Kanu, alipoibuka kidedea.
Yaya Toure alikuwa mchezaji muhimu wa Ivory Coast
wakati walipotinga robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka jana
na mbio za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil
mwaka huu, lakini Mikel alikuwa akipewa nafasi pia kutokana na kuisaidia
Nigeria kutwaa ubingwa wa Afrika na kufuzu Kombe la Dunia.
Tuzo nyingine zilitolewa kwa Stephen Keshi (Kocha
Bora) na kiungo wa Misri, Mohamed Aboutrika (Mwanasoka Bora wa Soka la
Ndani) huku tuzo ya gwiji la Afrika ikinyakuliwa na kocha, Bruno Metsu,
ambaye kwa sasa ni marehemu.
No comments:
Post a Comment